June 06, 2015

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kikitegemea kupata upinzani mkubwa kuliko wakati mwingine wowote tangu kuanza kwa siasa za mfumo wa vyama vingi nchini.
Wapinzani wakienda sawa kama wanavyodai na kumsimamisha mgombea mmoja kwa kila nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani, kazi itakuwa kubwa kwao.
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba mwaka jana ulitoa picha inayoonyesha kuimarika kwa upinzani nchini, kwani matokeo ya jumla yalionyesha kupanda kwa idadi ya viongozi wake huku wale wa chama tawala wakishuka.

Pamoja na upinzani huo kuonekana mkubwa, dalili zinaonyesha CCM, kwa mara nyingine, itashinda tena katika uchaguzi huu, kama ilivyoweza kufanya mara nne huko nyuma, katika chaguzi zote za 1995, 2000, 2005 na 2010.
Uzoefu wa chaguzi zote hizo unaonyesha kuwa mtaji mkubwa wa chama tawala umekuwa ni kura za vijijini, kwani kwa mijini wengi wanaonekana kuhitaji mabadiliko, ama kwa kutoridhishwa na mambo yanavyokwenda au kwa hulka tu ya binadamu ya kutotaka kitu kimoja kuwepo kwa muda wote pasipo kubadilika.
Bila kujali kama waishio mijini wanahitaji mabadiliko kwa sababu zipi, lengo langu hasa ni kuzungumzia nguzo kubwa ya kura za CCM, zinazopatikana kwa Watanzania waishio vijijini. Nimejaribu kutafuta namna nzuri ninavyoweza kuwazungumzia kwa kuwalinganisha na chama hiki, nimeona sina nyingine nzuri zaidi ya kuamini kabisa kuwa hawa wanadhihakiwa.
Wanadhihakiwa kwa sababu wao ndiyo wanaokiweka chama hiki madarakani, lakini wao ndiyo watu wa mwisho kabisa ambao wanatazamwa na serikali inayoongozwa na CCM. Linapokuja suala la masilahi, watu hawa hawatendewi vile ambavyo tungetarajia.
Kule vijijini tunawakuta wakulima na wafugaji, lakini watu hawa wanapata maumivu makubwa sana kutoka kwa serikali yao. Wao wanalima, lakini kilimo chao kinakuwa kigumu kutokana na sababu nyingi, lakini kubwa zaidi ni bei kubwa ya mbolea. Wanalima kwa ajili ya chakula na biashara.
Wanauziwa mbolea na pembejeo zingine za kilimo kwa bei kubwa na hakuna mtetezi. Serikali inajua kuhusu ukubwa wa bei hizi, lakini haifanyi juhudi zozote za makusudi kuwapunguzia mzigo huu mkubwa. Lakini kana kwamba haitoshi, wakishalima kwa gharama kubwa, angalia jinsi wafanyabiashara wanavyowadhulumu mazao yao sokoni.
Bei wanayouzia ni ile inayotajwa na wafanyabiashara na katika mazao ambayo yanauzwa kwa uzito wa kilo, wanaibiwa kwa sababu wafanyabiashara hawa wanaharibu mizani. Hii maana yake ni kuwa mzigo wa kilo mia moja, wanalipwa fedha za kilo 80!
Serikali inafahamu kwamba mazao ya wakulima yananunuliwa kwa bei ndogo na wafanyabiashara wanaharibu mizani. Hiki ni kilio chao cha miaka nenda rudi, lakini hakuna linalofanyika kuwasaidia.
Na kuhusu wafugaji, kila mmoja anafahamu jinsi wanavyohangaika na mifugo yao. Unapofika wakati wa kampeni kama huu, kila mwanasiasa, hukimbilia vijijini na kuwaahidi kumaliza matatizo haya, lakini wote ni mashahidi kuwa wameendelea kutaabika.

Kuna ujumbe mmoja muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi.
Kwa kadiri mambo yanavyokwenda, inaonekana kabisa wapinzani wameanza kulivamia kundi hili la wapiga kura za ndiyo kwa chama tawala. Siku hawa waking’amua kuwa wanadanganywa na

kuonekana wajinga, ni wazi kuwa huo ndiyo utakuwa mwisho wa CCM.
Isisubiri wakati huo ufike kwa sababu wapiga kura wataona mnawadhihaki. Baadaye mwaka huu mtawaendea na kuwapa maneno yaleyale ya mwaka 2010. Litakuwa ni jambo la kushukuru sana kama wataendelea kuwaelewa.
 Ikitokea hivyo na serikali nayo ikaendelea kuwa vilevile, sitaki kuamini kama mwaka 2020 wataelewa tena.

Related Posts:

  • Good News: Ibrahim Ajib apata mtoto   Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa familia ya Mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu, imejaaliwa kupata mtoto wa kike. Ajibu alishindwa kusafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Algiers, Algeria kwa ajili ya mechi y… Read More
  • Haji S Manara auingia mziki wa TFF, yamemkuta haya.   Mbwembwe za Haji Manara zimeanza kumponza. Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, imempa onyo kali Mkuu huyo wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba kwa kosa la kuingia uwanjani. Kiongozi huyo alifanya kos… Read More
  • Live: PM Katika Uzinduzi wa Daraja la Kilombero   RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 5, 2018 amezindua Rasmi Darala la Magufuli lililopo Kilombero mkoani humo. Katika hafla ya uzinduzi huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na ma… Read More
  • Video: Stamina afunga ndoa Morogoro   Mwanamuziki wa muziki wa Hip Hop kutoka mkoani Morogoro Stamina leo hii amefunga pingu zamaisha katika kanisa la Mtakatifu Patriki lililopo  mkoani hapa.          … Read More
  • ziara ya Magufuli Morogoro, Mwanafunzi ajitosa   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alipokua akiendelea na ziara yake mkoani Morogoro akielekea Kilombero amezungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’ula ambapo alisimama na kuzungumza na w… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE