

Swali: Fainali
ya UEFA itakuwa historia kubwa kati ya Barcelona au Jeventus. Wewe
umewahi kufanikiwa mwaka 2009, unaweza kusema chochote juu ya usiku wa
fainali ya UEFA?
TH: Ni ngumu sana kufanikiwa kushinda kombe, inatakiwa kuwa na umoja, uwezo na Imani ndani yenu, pia kuwa na hamu ya kushinda pamoja na kujitolea. Siamini juu ya bahati, chochote unachokifanya vizuri ni kwasababu una uwezo wa kukifanya vizuri. Kuna wakati utapata usaidizi mzuri kati ya wenzako kwenye timu lakini sio swala la bahati.
Swali: Unaionaje Barcelona hii na yenu?
TH: Sipendi kufananisha timu lakini naamini hivi sasa Barcelona wana team nzuri sana.
Swali: Timu hii ya sasa ya Barcelona unadhani ina wachezaji wazuri safu ya ushambuliaji?
TH: Nadhani hawa wa sasa hivi wameshinda magoli mengi, lakini ishu sio tu kufunga magoli mengi. Upande wangu ni zaidi ya magoli tu, unaweza kurudi nyuma kwenye historia ukaona wachezaji wazuri zaidi waliofanya vizuri pale mbele. Kinachotakiwa ni kuwa na balance nzuri pale mbele, nadhani hawa wa sasa wanayo hiyo balance.
Swali: Unadhani Juventus inaweza kuzuia mapacha watu pale mbele?
TH: Juventus
ipo vizuri sana kuanzia Alvaro Morato, Carlos Tevez na Paul Pogba. Kuna
Claudio Marchisio na pia tusimsahau Adrea Pirlo. Pia tunajua jinsi gani
Juve walivyowazuri pale nyuma na pia wanaweza kukaa na mpira pia.
Lakini kwenye hii fainali hawawezi kukaa na mpira zaidi ya Barcelona
japokuwa uwezo wa kuzuia wanao. Kwangu mimi timu yoyote inayotaka
kuzuia Barcelona inabidi wazuie timu nzima na sio mchezaji mmoja.
Swali: Unaamini Juventus wanaweza kubadilisha mawazo ya watu na kuwafunga Messi na wenzake?
TH: Chochote kinaweza kutokea kwenye fainali. Nakumbuka Juve Vs Madrid mwaka 98, kila mtu alijua matokea jinsi yatakavyokua lakini mambo yakawa tofauti. Fainali haitabiliki.
Swali: Unatuwa umekaa kwenye kiti unaangalia mechi kupitia Sky Sports, je utajiskia wivu kwasababu hauchezi ile mechi?
TH: Nimecheza
fainali nakushinda lakini nimecheza na kufungwa pia nikiwa na Arsenal.
Lakini ningejiskia vizuri kucheza fainali ya mwaka huu pia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment