July 27, 2015

Bobbi Kristina Brown, binti wa marehemu mwanamuziki Whitney Houston, amefariki akiwa na miaka 22, mwakilishi wa familia amesema.

Kristen Foster alisema alifariki siku ya Jumapili akiwa amezungukwa na familia yake na hatimaye “amepumzika kwenye mikono ya Mungu.”

Bobbi Kristina akiwa na wazazi wake Whitney Houston na Bobbi Brown mwaka 2004

Brown alikutwa hajitambui akiwa bafuni Januari 31 na kuwekwa kwenye hospitali ya coma. Hakuwahi kupata tena fahamu.

Alirudishwa nyumbani katika mji wa Duluth, Georgia, mwezi baada ya hali yake kuwa mbaya.

Bobbi Kristina akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Nick Gordon Agosti 2012

Brown alikuwa binti wa pekee wa Houston na mwimbaji wa RnB Bobby Brown.

Whitney Houston alikutwa amefariki katika bafu ya hoteli mjini Los Angeles mwaka 2012

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE