Mfalme wa masauti staa Christian Bella amesema kuwa hivi sasa anafanya
utambulisho mkubwa wa video ya wimbo 'Amerudi' na bendi yake ya Malaika
kama zawadi kwa mashabiki wake katika onesho kubwa la muziki kesho
jijini Dar es Salaam.
Bella anayeendelea kushika chati kupitia kazi zake zikiwemo 'Nashindwa',
'Nakuhitaji', na 'Amerudi,' ameongea na eNewz kuwa hivi sasa yupo
mbioni kufanya kazi mpya iitwayo 'Namgharamia' na staa wa muziki wa
Bongofleva.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment