Picha hii ni kwa hisani ya Maktaba ya Google
Baada
ya kufungiwa na mamlaka ya chakula na dawa kwa machinjio ya nyama ya
manispaa ya Morogoro,wachinjaji na wafanyabiashara wa Nyama katika
manispaa ya Morogoro wametishia kugoma kuendelea kutumia machinjio ya
sasa ya dharura ya dakawa wilayani Mvomero waliyopewa na mamlaka
husika,kwa madai kuwa eneo hilo ni mbali na gharama za ushuru
zimeongezeka.
Wafanyabiashara hao wa nyama wamelalamikia kufuata huduma hiyo ya
machinjio eneo la dakawa kwa madai ni mbali,na wanalazimika kufuata
umbali wa zaidi ya kilometa 80 kwenda na kurudi kutokea mjini sambamba
na usumbufu mwingine,na kwamba hali hiyo imekwenda sambamba na ongezeko
la gharama za ushuru,mambo ambayo ni hasara kwao kiuendeshaji na
yanachelewesha upatikanaji wa huduma kwa wakati.
Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Theresia Mahongo,alipohojiwa
kuhusiana na hatua hiyo na ile ya kufungiwa na TFDA baada ya ukaguzi wa
kushtukiza,amesema wanaendelea vyema na marekebisho na matengenezo ya
machinjio hayo yaliyofungiwa ili kukidhi vigezo na kwamba hadi kufikia
ijumaa ya wiki ijayo huenda wakawa wamekamilisha na kuendelea upya kwa
shughuli za sughuli za uchinjaji kama kawaida.
Siku ya jumanne wiki hii,mamlaka ya chakula na dawa TFDA ilifanya
ukaguzi wa kushtukiza katika machinjio ya manispaa ya Morogoro na
kulazimika kuifungia machinjio hiyo kutokana na dosari kadhaa
zilizojitokeza,ikiwemo kukithiri kwa uchafu,hali inayotishia usalama wa
watumiaji wa nyama,ambapo manispaa iliwataka wafanyabiashara kutumia
machinjio ya dakawa wilayani mvomero kwa dharura,lakini baadhi ya
wachinjaji wamegomea kwenda kutokana na umbali na sababu nyingine.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment