Wizi huo wa umeme umebainika kufuatia maafisa wa shirika la umeme
Tanesco mkoani hapa kufanya opersheni ya kuwasaka wateja
wanaojiunganishia umeme na kusababisha hasara kwa shirika hilo ambapo
akizungumza wakati wa operesheni hiyo mhandisi Mposheleye Mwasenga
amesema shirika limekuwa likipata hasara na kutokea majanga ya moto
katika maeneo mengi nchini kutokana na baadhi ya wateja kuiba umeme.
Aidha mhandisi Mwasenga amesema Tanesco haitasita kuwachukulia
hatua za kisheria wale wote wanaojihusisha na wizi wa umeme ambapo pia
amesema msako huo ni endelevu na kuwataka wananchi kutoa tarifa za watu
wanaolihujumu shirika hilo.
Kwa upande wao baadhi ya watuhumiwa wa wizi wa umeme waliokamatwa
wamekiri kuhusika na wizi huo ingawa wametupia lawama shirika hilo
kulimbikiza ankara za umeme kwa zaidi ya miezi mitatu bila kuwaletea
wateja wao hali inayosababisha wateja hao kushindwa kulipa kwa mkupuo
mmoja na hivyo kuamua kujiunganishia ili kuepuka gharama kubwa huku
wengine wakikana kuhusika na wizi huo.
Chanzo: itv.co.tz
0 MAONI YAKO:
Post a Comment