November 06, 2015

Hawa jamaa wawili kwa kweli kwa pamoja tunaweza kusema wamepeleka kiliomtaa wa Lumumba, waswahili husema kwa mjinga huenda kicheko lakini kwa mwelevu huenda kilio.

Ujio wa Lowassa UKAWA umepeleka kilio kikubwa sana CCM japo kuwa wanajikazakinyasa wanakufa na Tai shingoni. Majuzi Mh. January Makamba aliita waandishi wa habari na kujinasibu eti CCMimepata wabunge 176 mpaka sasa na kufanikiwa kugomboa majimbo 11 yaliyokuwa yawapinzani.

Sasa habu ona hapo chini kilio Lowassa alichokipeleka CCM ambacho Makamba hakupenda kutaja.

1. Viti maalumu vya CCM vimepungua kwa 40% toka 79bunge lilopita la10 mpaka 62 bunge la11. Wakati CHADEMA na CUF viti hivyo vimeongezeka haya ni maumivu makubwa

2. CCM imenyang`anywauongozi wa majiji 4 kati ya majiji 5imebakiwa na uongozi katika jiji moja tu la Mwanza,. Majiji yafuatayo CCM nichama cha upinzani , Jiji la Mbeya, Jiji kuu la Dar-es-Salaam, Jiji la kitaliila Arusha na jiji la Tanga ambalo ilikuwa ni ngome yao, ngome imevunjwa.

3. Ruzuku ya CCM imepungua kwa 40% kutokana na kuraza rais alizopata , mgao wa ruzuku utakuwa 60 kwa 40 kwa maana 58% alizopataRais Magufuri kwa desilimali ya karibu itakuwa 60, na 39.8% ya kura za Lowassaalizopata kwa desilimali ya karibu itakuwa 40. Kwa hiyo CHADEMA imeinya`anyaCCM 20% ya ruzuku, je! Siyo maumivu hayo?

4. Uongozi wa halmashauri ndiyo usiseme. Kabla yaLowassa halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na wapinzani zilikuwa 5 sasahalmashauli hizo zimeongezeika na kufika 30, katika halmashauri hizo CCMwatakuwa bachbancher.

5. Kilio kikubwa zaidi ni cha Zitto Kabwe alichowapaCCM katika halmashauri ya Kigoma/ujiji. Katika halmashauri hii hakuna mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa kutia pua, halmashauri hii ni mali ya Zitto Kbakwe kwamaana ya Meya hadi madiwani. Halmashauri hii mwenyekiti wa CCM au mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa wataenda kufanya nini? Wakati wakuu hao wameng`ang`anakumnyang`anya Kafulila ubunge wake huku nyuma Zitto anachukua halmashauri ya mjini,shame on them

6. Kuna kilio manispaa ya Mtwara/Mkindani na Mtwaravijijini kwa Hawa Ghasia, huenda Umeya wa Shilingi na wa Ndazigula umeotambawa.

Haya ndo ilitakiwa Mh. January Makamba ayaseme katika kile kikao chawaandishi wa habari alichokiitisha.

Source: ebaeban/Jamii Forums

Related Posts:

  • TUONANE JANWARY SHOW KUFANYIKA MORO JUMAPILIKama upo Morogoro tukutane uwanja wa K/NDEGE shule ya Msingi  jumapili hii tutakuwa na @officiallinah @fidq @staminashorwebwenzi @Shilolekiuno @yamotoband @Nikiwapili  @Mwanafa na list nzima hiyo hapo. Utakosaje sas… Read More
  • DIAMOND ULINZI MZITO UGANDA, AWEKEWA WAJEDA Mlinzi kutoka jeshi la Uganda Hawa askari tuliwaona wakati Diamond Platnumz amewasili Uganda na kupokelewa Airport kwa mbwembwe sana. Kumbe ulinzi wao uliendelea mpaka siku ya sho ambapo mmoja wao aliwekwa Nje y… Read More
  • VIDEO YA ALLY KIBA KUONESHWA KWENYE VITUO HIVI VIKBWA Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’imeanza kuonyeshwa ijumaa ya 19 Decemba 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Video imeta… Read More
  • WIMBO MPYA WA RAY C HUU HAPA    Ukiiskia sauti ya leo ya Ray c  huwezi kumtofautisha kabisa na Ray c yule wa kitambo, sauti ile ile na swaga zile zile. Hapa anakwambia Mshum  mshum. Huu niwimbo wake wa kwanza tangu aamue kurudi kat… Read More
  • NEW SONG// BAMBA- VENNT SKILLZ ft KENNI KENNIE  Hii ni ngoma mpya kabisa kutoka kwa mtayarishaji wa muziki mkoani Morogoro anayefanya vema kwa sasa katika anga ya muziki wa kizazi kipya ni Vennt Skillz wa kwanza Records hapa kamshirikisha mkali wa R $ B mkoani Mo… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE