THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Kwa mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja
na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa
sikukuu au mapumziko, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya
Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015,
yatumike kwa kufanya kazi. Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu
(2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi
(Uhuru na Kazi) katika Taifa letu. Mheshimiwa Rais ameelekeza
Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama
vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao
katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi
mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo
itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili
ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni
pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za
hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi
zitakavyoamua.
Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika
kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo, sherehe hizi
zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015
0 MAONI YAKO:
Post a Comment