Uamuzi huo ni hatua ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, kuwachukulia hatua watumishi wa taasisi za umma na serikali kutokana na uwajibikaji mbovu na uzembe kazini ulioisabishia hasara ya mabilion ya shilingi serikali .
Miongoni mwa hatua nyingine zilizochukuliwa na Rais Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa za kuzuia upotevu wa mapato ya serikali kwenye mamlaka ya Bandari ni kuwasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu ambao ni wasimamizi wanane wa Bandari kavu.
Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akiambatana na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anaeleza wengine waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi kuwa nia viongozi wanne wa mamlaka ya Bandari ambao walitoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari kwenda kwenye bandari kavu.
Kuhusiana na shirika la Reli Tanzania TRL juu ya matumizi mabaya ya fedha shilingi bilion 13 nje ya utaratibu, waziri Mkuu Majaliwa amesema licha ya kwamba uchunguzi unaendelea, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjaka uteuzi wake umetenguliwa na rais na kwamba atapangiwa kazi nyingine.
Novemba 27 mwaka huu Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es salaam ambapo alifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.
Pia Desemba 4 mwaka huu alirudi tena Bandarini akiwa na ripoti ya ukaguzi wa ndani ya Julai 30 2015 ya Mamlaka ya Bandari ambayo ilionesha ukwepaji kodi ikiwemo makontena 2387 yaliyopitishwa kati ya Machi – septemba 2014 kinyume cha utaratibu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment