Kampuni ya Apple imepinga agizo la mahakama la kuitaka kusaidiana na FBI katika uchunguzi wa washukiwa wa ugaidi.
Apple imemtaka jaji Sheri Pym wa mahakama ya California kufutilia mbali agizo hilo lililotolewa Februari 16 la kuitaka kampuni hiyo kufungua simu ya iPhone iliyokuwa ikitumiwa na Syed Farook.
Mkurugenzi mkuu wa Apple Tim Cook alitoa maelezo na kuarifu kwamba hatua ya kuisaidia FBI ni kinyume na kanuni za kulinda usalama wa wateja.
Apple sasa imeamua kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali kwa kuwashinikiza kukiuka sheria za kampuni.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment