February 28, 2016

 

Hillary Clinton ameshinda kwa wingi wa kura uchaguzi wa mchujo wa urais katika jimbo la South Carolina dhidi ya mpinzani wake mkuu katika chama chao cha Democratic Bernie Sander.
Bi Clinton alipata kura asilimia 84, miongoni mwa wapiga kura wengi ambao ni watu wenye asili ya Kiafrika katika jimbo hilo.
Aliahidi katika hotuba yake ya ushindi kuwa ataendelea kupigania kila kura katika majimbo yote yaliyosalia na kuwa hatapuuza lo lote.
Huku akigusia kura za mchujo za Jumanne Kuu au ijulikanavyo kama ''Super Tuesday'', Bi Clinton alisema kuwa kura hizo za uchaguzi sasa zimechukua mkondo wa kitaifa.
Bernie Sanders alimpongeza Bi Clinton kwa ushindi wake lakini akasema mambo bado.
Bi Clinton alimshinda Sanders kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.
Hii ikiashiria kuwa Clinton alipata kura 8 kati ya 10 zilizopigwa na wapigaji kura wamarekani weusi.
Ushindi huo ni wa tatu kwa bi Clinton katika kinyang'anyiro hichi cha kumtafuta mshika bendera wa chama cha Democratic.
Clinton alikuwa ameshinda majimbo ya Iowa na Nevada.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE