March 15, 2016

               

Na Mwashungi Tahir na miza Kona – Maelezo Zanzibar    

Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa  na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu na watu wasiojulikana  majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na  kujeruhi baadhi ya watu  waliokuwa wamelala  na kusababisha hasara kubwa.

Amesema tukio hilo linafanana na  lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya  uhalifu huo.

Akizungumzia  matukio  mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema  Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa  katika vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani amewatoa hofu  wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari katika maeneo  mengi ya mijini na vijijini  ni  moja ya juhudi za kuimarisha  ulinzi  na kuhakikisha  uchaguzi huo utakuwa salama na amani.

Ametahadharisha kuwa mtu yoyote atakayejihusisha kuanzisha vurugu au kufanya kitendo chenye ishara ya  uvunjifu wa amani atapambambana na vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani ametoa wito kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba bila ya woga  kwani jeshi hilo limejipanga  kuimarisha ulinzi  sehemu  zote.

                  

Related Posts:

  • MARKEL: TUTAWALINDA WAYAHUDI NA WAISLA,U UJERUMANI Kansela Angela Merkel   Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameahidi kuwalinda Wayahudi na Waislamu wanaoishi nchini Ujerumani dhidi ya ubaguzi. Amesema demokrasia ndiyo njia bora ya kupambana na machafuko yanayo… Read More
  • WATANZANIA WENGI WAFUNGWA HONG KONG Kasisi mmoja raia wa Australia amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania. Kasisi huyo John Wortherspoon ambaye … Read More
  • HUU NDIYO MPANGO MPYA WA THT 2015            Imezoeleka Tanzania House of Tallent (THT) imekua ikitoa wasanii peke yake ambao asilimia kubwa ya wasanii wengi wa Bongo Fleva wamepitia kwenye mikono ya Nyum… Read More
  • PAPA AWASILI UFILIPINO Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani,Mtakatifu Francis, amewasili nchini Ufilipino, nchi yenye Wakatoliki wengi zaidi barani Asia, huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa. Maelfu ya Wafilipino wamejipanga katika misur… Read More
  • RONALDO DE LIMA KUREJEA DIMBANI Ronaldo de Lima anavyoonekana sasa. Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima anatarajia kurejea tena dimbani. De lima ameahidi kupunguza… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE