Mkuu mpya wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini Kenya
(EACC) amesema theluthi moja ya bajeti ya nchi hiyo inapotea kutokana na
ufisadi.
Phili Kinisu, ameviambia vyombo vya habari kuwa Kenya inapoteza
theluthi moja ya bajeti yake ambayo ni sawa na takribani dola bilioni
sita kila mwaka na kuongeza kwamba tume yake inakabiliwa na uhaba mkubwa
wa wafanyakazi na vifaa vya kisasa vya kukabilina na tatizo la ufisadi.
Kinisu, ambaye alishika uongozi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi mwezi Januari mwaka huu baada ya mtangulizi wake kujiuzulu mwaka uliopita amesema bajeti ya serikali inakaribia dola bilioni 20, sawa na karibu shilingi trilioni mbili na kuongeza kuwa theluthi moja ya fedha hizo zinapotea kupitia vitendo vya ufisadi.
Kinisu, ambaye ni mkaguzi wa hesabu mstaafu amesema anataka kuyafanyia kazi manung'uniko ya Wakenya dhidi ya ufisadi lakini amesisitiza kuwa kampeni ya kulitokomeza tatizo hilo inapasa itokane na mashinikizo ya wananchi wenyewe ya kutaka mabadiliko.
Wakati Waziri wa Fedha wa Kenya Henry Rotich amepinga makisio hayo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa EACC juu ya upotevu wa fedha za bajeti ya serikali, Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amekiri kuwa ufisadi umefikia kiwango cha kuhatarisha usalama wa taifa.
Kenya ina historia ya kashfa za mamilioni ya dola ambazo zimeshindwa kuwatia hatiani wahusika wakuu, suala ambalo limewakasirisha wananchi ambao wanawatuhumu maafisa waandamizi kuwa wanafanya vitendo vya ufisadi bila ya kuchukuliwa hatua na kuwashajiisha walio chini yao kujihusisha na vitendo hivyo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment