March 06, 2016

Watatu wauawa kwa mripuko wa bomu nchini Somalia
Kwa akali watu watatu wameripotiwa kuuawa katika miripuko iliyotokea leo kusini mwa Somalia.
Miripuko hiyo imetokea katika eneo la Bardera mjini Gedo, kusini mwa Somalia ambapo kwa akali watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Kwa mujibu wa mashuhuda wa shambulio hilo, miripuko hiyo ilitokea katika barabara kuu ambayo mara nyingi hutumiwa na askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika AMISOM, kutoka Ethiopia. Inaelezwa kuwa, shambulizi hilo lililokuwa limewalenga moja kwa moja askari hao wa kusimamia amani nchini Somalia, liliwapata raia na kupelekea raia wa kawaida kupoteza maisha na kujeruhiwa. Licha ya polisi kuanzisha uchunguzi wa hujuma hiyo, imelinyoshea kidole cha lawama kundi la kigaidi la ash-Shabab kwa kuhusika na jinai hiyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo Mkuu wa Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Pembe ya Afrika, Peter de Clercq amesema kuwa, watoto wapatao 60,000 nchini Somalia wanakabiliwa na hatari ya kifo kutokana na uhaba wa misaada ya kibinadamu nchini humo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE