May 19, 2016

Tanzania Itasafa Sana Kuongezewa Uwakilishi CAF

Kumeanza kuzuka minong’ono mbalimbali nchini kuhusu uwakilishi wa Tanzania mwakani kwenye michuano ya klabu inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na hii ni mara baada ya Yanga kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano Kombe la Shirikisho Afrika jana.

Yanga imefuzu hatua hiyo mara baada ya kuitupa nje Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, ikipigwa ugenini 1-0 lakini ushindi wa 2-0 walioupata nyumbani uliwabeba Wanajangwani hao.
Minong’ono iliyoanza kuzuka ni kuwa, Simba itapanda ndege mwakani kupitia mgongo wa Yanga wa kufika hatua hiyo kwenye michuano ya CAF.
Lakini minong’ono hii ni sawa na ndoto za alinacha kutokana na kanuni za michuano hiyo kuibana Tanzania na nchi zote za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) isipokuwa Sudan tu, ambayo ndiyo imekuwa mkombozi wa ukanda huo kwa kuwa na rekodi ya kufanya vizuri.
Najua unataka kujua nini hicho hasa kinachoibana Tanzania na nchi za CECAFA kwa ujumla isipokuwa Sudan, jibu ni moja tu hakuna hata nchi moja iliyoweza kufikisha pointi 12 au kuendelea zinazohitajika ili Taifa fulani liweze kuongezewa timu kutoka moja hadi mbili katika kila michuano ya CAF ngazi ya vilabu.
Hiyo inatokana na timu za wawakilishi za ukanda huo kutokuwa na rekodi ya kufanya vizuri ndani ya michuano hiyo mara nyingi zikiishia raundi za awali ambazo hazina pointi, kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotolewa na CAF kuanzia mwaka 2010 -2014 na vijavyo vya miaka mitano mingine ijayo vitatolewa 2018 na hivi vitaangalia zaidi matokeo.
Rekodi ya viwango hivyo vya CAF inaiumbua ukanda wa CECAFA kwani hakuna hata nchi moja ukiiondoa Sudan, iliyoweza kujinyakulia hata pointi moja kutokana na kufanya huko vibaya ndani ya michuano hiyo.
Sudan yenyewe imekuwa ikibebwa na timu kongwe za huko El Merreikh, Al Hilal, ambazo zimeifanya nchi hiyo kufikisha jumla ya pointi 33 wakiwa nafasi ya tano kwa mujibu wa viwango vya CAF na hiyo ni kutokana na kufanya vizuri kwa timu zake hizo.
Kwa Yanga kuingia hatua ya makundi (robo fainali) ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu, sasa kunaihakikishia Tanzania kuandika pointi moja na sasa ikidaiwa pointi nyingine 11 ili iweze kuongezewa timu moja moja katika kila michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.
Yanga ikiingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo basi itakuwa na uhakika wa kuifanya Tanzania kuwa na alama mbili na ikifika fainali basi nchi hiyo itajikusanyia pointi tatu kama timu hiyo itapoteza fainali na pointi nne kama Wanajangwani hao wakiibuka mabingwa.
Kwa Afrika ni nchi 12 pekee ambazo zimejihakikishia nafasi ya kuingiza timu mbili mbili katika kila michuano hiyo CAF, Tunisia ikiwa kinara, ikifuatiwa na Misri, Congo DR, Algeria, Sudan, Ivory Coast, Morocco, Cameroon, Congo Brazzaville, Mali, Nigeria na Afrika Kusini, iliyoanza kufanya vizuri kwa miaka ya hivi karibuni.
Ni mtihani mkubwa sana kwa Tanzania na nchi za CECAFA inaotakiwa kuhakikisha inaufanya ili nchi wanachama ziweze kuongezewa uwakilishi katika michuano hiyo na ni lazima zisafe sana kuweza kufikia mafanikio waliyofikia timu hizo 12.
Kwani ili ujihakikishie ubora wewe mwenyewe na nchi yako kufika huko ni lazima uweze kupambana vilivyo na mataifa hayo 12 yanayoongoza kwa ubora katika ngazi ya klabu barani Afrika, la sivyo kila mwaka tutaishia kupeleka timu moja moja.
Kimahesabu ndani ya miaka miwili ijayo kwa upande wa Tanzania, ili tuweze kupeleka timu mbili mbili katika kila michuano ni lazima Yanga mwaka huu ihakikishe inaingia fainali na kuchukua kombe la michuano hiyo ili iihakikishie nchi pointi nne.
Na pia mwakani Yanga (Ligi ya Mabingwa) na Azam FC (Kombe la Shirikisho) zitakazoliwakilisha Taifa katika michuano hiyo zihakikishe zinachukua makombe ya michuano hiyo. Hii itaifanya Tanzania kupeleka timu mbili mbili (nne) mwaka 2018 katika michuano hiyo.
Imeandaliwa na ABDUCADO EMMANUEL.

Souce: Times Fm

Related Posts:

  • Hussein Bashe atuma salam za siku ya muungano   Mbunge wa Nzega mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Hussein Bashe, ameungana na watanzania katika maahimisho ya siku hii ya muungano kwa kutuma salam zake kwa taifa letu. Kupitia twitter Mh: Bashe ame tweet … Read More
  • Rais Magufuli na msamaha wa wafungwa siku ya Muungano Katika kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano… Read More
  • Live Match : Barcelona VS Osasuna   Ligi Kuu nchini Ispania inaendelea tena muda huu ambayo inawakutanisha Barcelona wanapambana dhidi ya  Osasuna. Fwatilia hapa uapate kujua matokeo ya mchezo huo.        … Read More
  • Serena: Sikutaka watu wajue nina mimba   Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat. Bingwa huyo wa taji la Grand slam mara 23 alichapisha picha katika mtandao huo wa kijamii akijiangalia katika… Read More
  • Wenger: Sitamuuza Sanchez kwa wapinzani wangu   Alexi Sanchez   Mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez hatouzwa kwa kilabu ya ligi ya Uingereza kulingana na mkufunzi Arsene Wenger. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chile, ambaye alifunga bao la… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE