Mkazi wa jijini Dar es Salaam akiwa na mfuko ukiwa na simu
Orijino baada ya kununua katika Gulio la siku mbili la
simu,Lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Makao makuu
ya kampuni hiyo,Mlimani City
Usiku wa kuamkia June 17 ulikuwa mbaya kwa baadhi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini. Wale waliokuwa wakimiliki siku feki walijikuta wakikosa mawasiliano na watu wao wa karibu baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA kuzima simu feki zaidi ya laki sita.
Wananchi hawa ambao simu imekuwa kiunganishi muhimu na ndugu, jamaa na marafiki pamoja na biashara zao, walijikuta wakimiliki makopo tu. Hiyo iliashiria kuwa wanatakiwa kujichanga tena ili kuweza kununua simu mpya na kurejea hewani, lasivyo mambo hayendi.
Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam,Wakiingia katika eneo la Makao Makuu ya Vodacom Tanzania,Mlimani City kujipatia simu Orijino kwenye Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki
Katika kipindi hicho ambacho wananchi hawa wamekuwa wakihaha, kampuni ya Vodacom Tanzania iligekuwa kuwa mkombozi wao kwa kuwaandalia gulio la simu orijino na za bei nafuu.
Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo cha EFM, Swebe Santana ni miongoni mwa wahanga waliofika kwenye gulio hilo kununua simu hizo.
“Mimi ni miongoni mwa wahanga ambao wamepata tabu kidogo ile tarehe 16 simu zikashake kidogo, zikasumbua lakini mimi nikasema mimi ni mwanafamilia wa Vodacom nifike pale niweze kununua simu orijino, asante sana Vodacom,” alisema Vodacom.
Kwakuwa bado TCRA inaendelea na mchakato wa kuzima simu feki zilizokuwa 2.6% ya simu zote nchini, wananchi wengi wataathirika na Vodacom imeahidi kuendelea kuwa mkombozi wao kwa kuwapa simu orijino.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment