Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema msanii huyo alihojiwa juzi kituoni hapo na yupo nje kwa dhamana, huku jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.
“Ni kweli juzi mchana tulimhoji Ney wa Mitego na yupo nje kwa dhamana kuhusu kukamatwa kwake nitatoa taarifa kwa nini tulimkamata,”amesema Kamanda Sirro.
Hata hivyo, Bongo5 imejaribu kumtafuta rapper huyo wa wimbo ‘Pale
Kati Patamu’ bila mafanikio, kwani kila akipigiwa kupitia simu yake ya
mkononi haipatikani.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment