August 01, 2016

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitasita kuwaondoa katika nyadhifa zao Wakurugenzi wote watakaoshiriki katika kutoa taarifa za uongo kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.


“Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo  kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakiandika taarifa za uongo kuwa mradi umekamilika wakati haujajengwa, hivyo wakurugenzi watakaoshiriki kutoa taarifa zisizokuwa sahihi wataondolewa,” alisema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana jioni (Jumapili, Julai 31, 2016) wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Alisema alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakurugenzi katika halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatembelea miradi yote inayojengwa katika maeneo yao ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama thamani yake inalingana na kiasi cha fedha kilichotolewa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali aihitaji Halmashauri kutoa ajira za mikataba kwenye kada zilizopo katika muundo wa ajira hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya mapitio ya watumishi wa mikataba.

“Tumeruhusu kuajiri kwa mikataba walimu wa masomo ya sayansi kwa kipindi cha miaka miwili tena kwa waliostaafu. Kuna kada zilizoko katika muundo wa ajira hizo hatuhitaji watumishi wa mikataba wakiwemo madereva msiwatumikishe kwa mikataba watakosa stahili zao,” alisema.

Akizungumzia suala la watumishi hewa mkoani Morogoro Waziri Mkuu alisema ni vema wakaendelea kufanya uchunguzi na ifikapo mwisho wa mwezi huu wawe wamekamilisha taarifa na kuanza kuchukua hatua kwa waliohusika kwa waliohusika.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe katika taarifa yake aliyoiwasilisha kwa Waziri Mkuu alisema mkoa unaendelea kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuzitaka taasisi zote za Serikali kufanya uhakiki wa mishahara hewa na malipo batili ya watumishi.

Alisema mkoa umebaini watumishi hewa 315 ambao wameisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 2.132 ambapo timu ya uhakiki bado inaendelea na zoezi hilo na taarifa kamili itatolewa mara kazi hiyo itakapo kamilika

Related Posts:

  • Hit Song:Watabamba - Jimmy flavour ft Blacqboi beats Jimmy Flavour ni mmoja ya wasanii toka mkoani Morogoro. amefanya nyimbo kadhaa na zikafanya powa sana ndani ya Morogoro. nyimbo kama Zohari,usingoje nikifa, na kushirikishwa nyimbo kadhaa na msanii Agatha Mbale. Lakini … Read More
  • Kombe la Shirikisho Afrika, Azam kanyaga twende   Klabu ya Azam imefuzu hatua ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi Complex, Dar es Salaam. Mabao ya Az… Read More
  • Audio: Simanzi - CN Record Huu hapa ni wimbo mwingine wa Maombolezo kufuatia ajali ya Roli la Mafuta Msamvu Morogoro iliyopoteza uhai wa zaidi ya watu 75 … Read More
  • Never Forget Moro - Hoodbangerz Kufuatia tukio la ajali ya Moto uliosababishwa na Roli la Mafuta na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 75 mkoani Morogoro, tukio lililotokea 10 August 2019 siku ya Jumamosi katika eneo la Msamvu, wasanii wa Hood Bangerz … Read More
  • Klabu Bingwa Afrika,Yanga yasonga mbele   Klabu ya YANGA imefuzu hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Towship Rollers ya Botswana. Bao la Yanga SC limefungwa na Juma Balinya ka… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE