Dayna Nyange amefunguka sababu ya kushindwa kufanya collabo muda wote na wasanii ambao ni rafiki zake kutoka nje.
Miezi kadhaa iliyopita muimbaji huyo alidai kuwa ana urafiki wa
karibu na baadhi ya wasanii kutoka nchini Uganda akiwemo Cindy, Alicios
na wengine wengi.
Akiongea na Bongo5, Dayna amesema kuwa amekuwa na mipango hiyo ya
kufanya nao collabo wasanii hao ambao ni watu wake wa karibu ila mpaka
pale mipango yake itakapokuwa sawa.
“Mipango ninayo ila sina haraka sana na hilo kwa kuwa nikiwa na
utayari kila kitu kitakuwa sawa niko na malengo kadhaa yakitimia ndio
nitapiga hatua nyingine,” amesema Dayna.
Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Komela’ ambao amemshirikisha Bill Nas.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment