Miss Tanzania 2004 ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Shule Direct, Faraja Kotta Nyalandu akishirikiana na benki ya NMB wamezindua mpango utakaotoa elimu ya fedha kwa wanafunzi wa shule za Sekondari ambao utawasaidia kufikia ndoto zao.
Mpango huo utawasaidia wanafunzi kupata elimu ya masuala ya fedha na utunzaji wa fedha kutoka NMB kupitia mtandao wa Shule Direct pamoja na kupata nafasi ya kufunguliwa akaunti ya kuweka fedha ambayo imepewa jina la ‘NMB Chipukizi Akaunti’.
Akiongea na waandishi pamoja na wanafunzi hao, Mhe. Mavunde ameupongerza mpango huo kwa kudai kuwa utawasaidia wanafunzi wengi endapo watauzingatia kwa kuwa takwimu zinaonyesha watu wengi hawana elimu ya fedha.
“Womens World Banking umebainisha kuwa watu wengi hawana elimu ya kutunza fedha na kwamba ufahamu wao wa fedha ni mdogo sana. Tukifanya matumizi sahihi ya fedha kwa kiasi kidogo unachokipata badala ya kufikiria kwenda kubet na kucheza kamari, fedha hiyo uwekeze ukanunue vitabu vya literature na sayansi viwasaidie.”
Naye Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu amesema, “Ni muhimu sana kwa mwanafunzi akajifunza masomo mengine ya ziada kama hii elimu ya fedha ili aweze kujua ana wajibu katika utunzaji fedha lakini pia kufanikisha ndoto zake kupitia hiyo elimu.”
Faraja ameongeza kuwa mpaka sasa wameshawafikia wanafunzi zaidi ya laki tatu tangu alipoianzisha taasisi hiyo mwaka 2013 na kwa wanaohitaji kujifunza zaidi wanatakiwa kutembelea mtandao wao wa www.shuledirect.co.tz.
Aidha Kaimu Meneja Muandamizi wa huduma za ziada na Bima kwenye kampuni ya NMB, Stephen Adili amesema kuwa wameamua kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi ili waweze kutambua umuhimu wa kujiwekea malengo yao kwenye masuala ya kifedha ili waweze kufikia ndoto zao.
Wakati huo huo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Benjamini Mkapa, Gebo Lugano ameishukuru NMB na Shule Direct kwa kuanza kutoa elimu hiyo ambayo itawafanya wanafunzi wawe makini kwenye kujiwekea akiba.
Baadhi ya wanafunzi waliojibu vizuri maswali wakisaini fomu za NMB
0 MAONI YAKO:
Post a Comment