MBUNGE wa Singida Mashariki
ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu,
amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa
Iblahim Lipumba amekosa hoja ya kuzungumza na badala yake anawavuruga
wanachama wa CUF.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa
Chadema amesema Lipumba hakuwahi kuwa na idadi kubwa ya wabunge kama
walivyo sasa tangu alipoanza kugombea urais zaidi ya kupata viti viwili
tu lakini walipoungana mwaka jana katika umoja wao wa Ukawa wakaibuka
na viti 10.
Kauli hiyo ameisema leo jijini Dar es
Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo aliongeza kuwa Lipumba
aache kukiandama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai
ya kuwa kinaivuruga CUF.
Aliongeza kuwa Lipumba kuendelea kutoa
matamshi hayo kwa wanachama wa CUF ni chanzo cha yeye kuendelea
kukivuruga chama hicho hivyo wanachama wampuuze kwani alikikimbia tokea
walipoungana katika umoja wao wa Ukawa kabla ya mwezi mmoja kujiunga
aliyekuwa mgombe urais kupitia umoja huo, Edward Lowasa kupitia Chadema.
Lissu akisikiliza kwa makini maswali aliyokuwa akiulizwa na wanahabari.
Kwa upande mwingine Lissu amesema
viongozi wa Chadema wamepanga Jumanne wiki ijayo kupelekea malalamiko
yao katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili wafuasi 10 wa Chadema
waliokamatwa kwa madai ya kusambaza maneno ya uchochezi.
Viongozi hao wakiendelea kusikiliza maswali ya wanahabari yaliyokuwa yakiulizwa.
Alisema wanapeleka hoja hiyo mahakamani ili mahakama iweze kuamuru waachiwe huru kwani hivi sasa wanateseka mahabusu.
Mkutano ukiendelea na wanahabari.
Alisema mahakama ndiyo chombo kikuu
chenye dhamana ya kuwahoji Mkuu Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu na
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DCI, Diwan Athumani ili watoe sababu ya
jeshi la polisi kuwaweka mahabusu wanachama 10 wa chadema kwa zaidi ya
wiki moja sasa bila kuwapeleka mahakamani.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment