Siku
kadhaa kabla ya kufanyika mkutano wa Yanga, Kamati ya Mwafaka ya Wazee
wa Yanga imezungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo ambao
mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji anataka autumie katika kuingia mkataba
wa miaka 10 kuimiliki nembo ya klabu.
Katibu
wa Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimalia amesema
ambacho Manji anakifanya kinaweza kusababisha timu hiy ikaingia katika
vurugu ambazo hazikuwepo kwa muda mrefu kwa sababu njia ambayo anatumia
inawagawa wanachama na mashabiki kwa wengine kuutaka mfumo na wengine
kuukataa.
“Hatutaki
kurudi kule tulipokuwepo katika mgogoro wa miaka saba, mwaka 2003 ndiyo
tukapata usuluhisho na kukubaliana kuwa litumike jina ambalo
lilikubaliwa na waasisi wetu, tukakubaliana kuwa kuwe na Yanga SC na
Yanga Cooperation,
“Yanga
kampuni ilifishwa na kukawa na utaratibu kuwa kuwe na hisa, Yanga SC
kuwe na hisa 51 na wanachama wawe na asilimia 49, na tulizunguka mikoa
mingi ili kufuta mgogoro uliokuwepo na kuomba ridhaa ya wanachama wa
klabu kukubali hisa,” alisema Akilimali na kuongeza.
“Tulipata
mwenyekiti mpaka anatoka timu ilikuwa na Mil. 200, tukampata bwana
Nchunga yeye akajiuzulu baada ya miaka miwili, tukamchagua Bwana Manji
akaongoza kwa miaka miwili, kwasababu tu ya upenzi ikabidi tuikanyage
katika akaongeza muda, ili tujipange na yeye ajipange ili tutafute
kuongozi wa baada yake, na tukafikia hatua ya kumchagua kwa mara
nyingine,
“Haijafika
hata miezi nane imeibuka swala la deni la Bilioni 11 na laki sita,
jambo ambalo limetushtusha sana wanayanga, limekuja tamko la mwenyekiti
kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na lebo yake kwa muda wa miaka 10,
kwasisi wote tunasema Yanga ni kubwa sana, Yanga haiwezi kukodishwa kama
masufuria ya kwenda shughulini. Kupitia mimi na wazee wa kamati
tumesema hatukubaliani na hilo”
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga, Mohammed Msumi.
Nae
aliyekuwa Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga, Mohammed Msumi amesema
kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na klabu ni vyema akakaa
pembeni na kuanzisha timu yake mwenyewe na kuacha Yanga iendeshwe na
mfumo ambao umezoeleka.
“Kwanini
anataka hili jambo haraka haraka na wakati alisema Yanga inajiendesha
kwa hasara, mfanyaniashara gani anakaa sehemu ya aina hiyo, kama hawezi
kufata utaratbu anaweza kuanzisha timu nyingine sio kuitaka yanga na
kutumia mamlaka kwa mabavu ili tu aipate Yanga,” alisema Msumi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment