Dj wa Clouds FM, D-Ommy, amedai kuwa kujituma na kuwa na show nyingi nje na ndani ya nchi, kumemsaidia kuonekana zaidi hadi kumfanya ashinde DJ bora wa Afrika kwenye tuzo za Afrimma 2016 zilizotolewa Jumamosi mjini Dallas, Marekani.
Ommy ameiambia Bongo5 kuwa tuzo hiyo imedhihirisha kuwa jitihada kwenye kazi yake hiyo haziendi bure.
“Nadhani kuwa na activities nyingi, hicho ni kitu ambacho kimenisaidia sana, yaani kwa mfano kuwa na shows nyingi na kubwa,” amesema Ommy. “Lakini pia kuwahudumia wananchi wangu wa Tanzania na nje ya Tanzania kupitia mixtape zangu, 5 Minutes of Dj D-Ommy, Washa Washa video mix. Na watu kunipigia kura kwa wingi sana,” ameongeza.
D-Ommy amesema kushinda tuzo hiyo kunamfanya aendelee kujituma na kuongeza ubunifu zaidi. Kwenye kipengele chake, alikuwa akishindana na Madj nguli wa Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment