November 18, 2016


Usiku wa Alhamisi ya Novemba, 17 kumefanyika halfa ya utoaji wa tuzo ya Forbes Person Of the Year kwa mwaka 2016 ambazo zilikuwa zikiwashirikisha watu watano kutoka mataifa mbalimbali Afrika.

Mmoja wa washirki wa tuzo hizo alikuwa ni Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ambaye alikuwa akishindana na Michiel Le Roux – mwanzilishi wa benki ya Capitec ya Afrika Kusini, Thuli Madonsela – mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu wa Afrika Kusini, Rais wa Mauritian, Ameenah Gurib na watu wa Rwanda.

Katika halfa ya utoaji wa tuzo hizo, Mwanasheria na mtetezi wa jamii wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Forbes Person of the Year 2016 kutokana na juhudi zake anazozifanya za kusaidia jamii ya watu wa Afrika Kusini katika mambo mbalimbali yakiwepo ya kisheria.

Thuli Madonsela anakuwa mshindi wa sita wa tuzo hizo tangu zianzishwe mwaka 2011, washindi waliopita walikuwa ni Sanusi Lamido Sanusi – 2011, James Mwangi – 2012, Akinwumi Adesina – 2013, Aliko Dangote – 2014 na Mohammed Dewji – 2015.

Kwa kushindwa huko kwa Rais Magufuli, Mohammed Dewji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) anasalia kuwa Mtanzania pekee ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo

Related Posts:

  • Polisi jela kwa kumuua mwanaharakati    Polisi wawili nchini Rwanda, wamefungwa miaka 20 jela kwa kumuua mwanaharakati wa kupinga ufisadi, aliyekuwa anachunguza kashfa ya ulanguzi wa madini mpakani. Gustave Makonene, aliyekuwa anafanya kazi na sh… Read More
  • Wafugaji wafunga minada ya mifugo Morogoro    Wafugaji jamii ya wamasai na wabarabaigi mkoani Morogoro wamefunga minada yote ya kuuza mifugo mkoani Morogoro kwa muda usiojulikana wakilalamikia serikali kushindwa kukomesha vitendo vya uon… Read More
  • UKAWA yatangaza kususia Kura ya Maoni   Vyama vya Siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) leo vimetangaza rasmi kuwa vitasusia kushiriki kura ya maoni, kwa ajili ya kupitisha Katiba mpya April 30, 2015 Vyama vya Sias… Read More
  • PROF. Muhongo aachia ngazi, Zitto Kabwe ampongeza kwa uamuzi huwo  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake hii leo kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow. Prof. Muhongo ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano wake na waa… Read More
  • Lulu Michael amlilia msanii Marlaw      Muigizaji Lulu Michael ambae ambaye kwa sasa bado anatamba na movie yake ya 'Foolish Age' amefunguka na kuonyesha hisia zake za ndani kwa mwanamuziki   Marlaw ambae alishawahi kutamba na hit… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE