November 21, 2016



Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemuomba radhi Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio.

Wakili Mwita alifanya hivyo jana baada ya hakimu huyo, Thomas Simba kumuhoji sababu za kushindwa kutekeleza amri hiyo wakati hati ya kumkamata ilitolewa Novemba 3, 2016 na wakili huyo kuisaini. “Kwa nini hamkumkamata” Si mlikuwa na wajibu wa kumkamata? Mnamuogopa?” alihoji hakimu huyo.

Hata hivyo, pamoja na kuomba radhi hiyo mahakama imechukua hati ya kusafiria ya Lissu ili kudhibiti safari zake nje ya nchi kwa kuwa amekuwa akisafiri bila kuitaarifu mahakama.

Katika kesi hiyo, Lissu na watu wengine watatu wameshtakiwa kwa makosa matano ya uchocheza kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti la Mawio kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2016 na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kabla ya uamuzi huo, Wakili Mwita alisema jana ilikuwa siku ya kesi hiyo kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kukamilika.

Kuhusu madai ya kudharau mahakama Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lissu aliiambia mahakama kuwa mteja wake yupo mahakamani, hivyo ametii amri ya mahakama na kwamba jukumu la dhamana ni kuhakikisha mshtakiwa anakuwapo mahakamani wakati wa kesi yake na kwamba uwepo wake ni kutii masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Wakili Mwita alidai kuwa kitendo cha Lissu kutofika mahakamani mara mbili mfululizo ni kama kuonyesha dharau kwa mahakama hiyo.

Mwita alidai kuwa Lissu ni mwanataaluma wa sheria na anafahamu taratibu za kufuatwa kama hafiki mahakamani na kwamba mdhamini si mbadala wa mshtakiwa mahakamani.

“Alipaswa kuandika barua kuitaarifu mahakama hii kama wakili kuwa ana kesi ya uchaguzi anayoiendesha Bunda na kuambatanisha na samansi ama orodha ya kesi. Tunaomba mahakama iheshimiwe na jukumu la kumfutia dhamana ama kutokumfutia dhamana Lissu bado lipo mikononi mwako mheshimiwa,” alieleza wakili huyo wa Serikali.

Akizungumzia hoja hizo, Hakimu Simba alisema Lissu ni wakili maarufu, msomi na anajua taratibu zote za mahakama, lakini wadhamini wake wanababaika, hivyo alimtaka aeleze sababu za kwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani.

Lissu alijibu kuwa hakuwa na nia ya kuidharau mahakama, wala kuikimbia kesi inayomkabili bali alikwenda Ujerumani katika mazingira ya dharura.

Hakimu Simba alimwambia mahakama inafahamu kesi za uchaguzi na maelekezo yake, hivyo ikamuuliza sababu za kutotoa taarifa wakati alipokwenda kushughulikia kesi ya Bunda 

“Nilipopata taarifa ya kwenda kuiendesha kesi hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya kutoka nchini Ujerumani na kwamba niliandika barua ya kuitaarifu mahakama na nilituma iletwe mahakamani kupitia wasaidizi wangu,”alisema Lissu.

Lakini Hakimu Simba alisema: “Hakuna barua iliyotufikia. Usituingize katika migogoro kutokana na nafasi yako katika jamii ya mwanasheria. Hatukuogopi labda upande wa mashtaka ndio wamekuogopa.

“Tunataka kufuata mfumo, hatutakuogopa na wala hatutakuonea. Hapa naona upande wa mashtaka wanapiga blaa blaa, tuelewane tunaichukua hati yako ya kusafiria ili ukitaka kusafiri tujue.”

Related Posts:

  • Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi   Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi  Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi . Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AF… Read More
  • Watanzania watakiwa kudumisha amani   Viongozi wa dini, wanasiasa na wazee nchini wamewaonya Watanzania kujiepusha na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani. Viongozi hao walisema hayo, Dar es Salaam jana katika Mkutano kuhusu Amani na Utulivu wa T… Read More
  • Uganda wapo tofauti na sisi katika video: Mr Blue   Msanii Mr blue ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya kufanya video na msanii Navio kutoka Uganda alifunguka na kusema kuwa ameona tofauti kubwa sana katika ufanyaji wa video bongo na nch… Read More
  • Ulikosa kuangalia interview ya NAY wa Mitego na Sporah? Ingia hapa sasa    Ney Wa Mitego is a Bongo Flava artist from Tanzania   We talked about his life style, his music world and how he became as single parent raising his son of just few months. Ney say he made the choi… Read More
  • Sterling apata mtetezi   Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ametetewa kwa kuwa na hamu kujiunga na vilabu vikubwa. Mshambuliaji huyo wa Liverpool huenda asilaumiwe kwa kuonyesha hamu ya kung'aa zaidi na kutaka kushinda vikombe. Hii ni kw… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE