Baada ya kuachiwa kwa dhamana Jumatatu hii, Vanessa Mdee ametakiwa kuripoti kituo cha polisi cha kati (Central) Jumatano hii.Kwa mujibu wa maelezo ambayo Bongo5 imepatiwa kutoka kituoni hapo, hitmaker huyo wa Cash Madame ameachiwa kwa dhamana Jumatatu hii, baada ya kufanyiwa mahojiano ya mwisho hiyo jana.Mrembo huyo amekuwa akishikiliwa na jeshi la polisi tangu Jumatano iliyopita. Vanessa ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana kuhusishwa na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
RC SHINYANGA AIPONGEZA KISHAPU UPANDAJI MITI, ATOA WITO WA KULINDA MUUNGANO
-
Na Sumai Salum -Kishapu
Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wamehimizwa kuendelea kuulinda na kuuenzi
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa misingi ya undugu, u...
4 hours ago





0 MAONI YAKO:
Post a Comment