April 07, 2017

Wanajeshi MK 
Maandamano ya vyama vya upinzani Afrika kusini pamoja na kundi linalo jiita Save South Africa yameanza katika kumshinikiza Rais Jacob Zuma ang'atuke madarakani.
Maandamano hayo yamepangiwa kufanyika nchi nzima.
Wanajeshi wa uMkhonto we Sizwe maarufu MK wametawanywa kushika doria nje ya makao makuu ya chama cha ANC mjini Johannesburg.
Waziri anayeshughulika na masuala ya polisi nchini awali amewaonya wale wote watakao fanya fujo na kuharibu mali ya umma, sheria itafuata mkondo.Zuma ameponea katika siku za nyuma wito wa kumtaka ajiuzulu.
Aliungwa mkono hivi juzi na kamati kuu ndani ya chama chake cha ANC.
Ilikuwa inachunguza malalamiko yaliowasilishwa na baadhi ya maafisa wa juu wa chama hicho kwamba Jacob Zuma hakushauriana nao kuhusu suala la kufanyia baraza la mawaziri mageuzi.
Shutuma kali zimeibuka kufuatia mageuzi hayo, zaidi kufuatia kutimuliwa kwa waziri wa fedha nchini anayeheshimika na wengi, Pravin Gordhan.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa Jeshi la polisi nchini imeeleza kuwa maandamano hayo ya kwenda kwenye ikulu ya Rais hayana kibali, ambacho kimewaruhusu kufika huko.

Related Posts:

  • Spika wa bunge ajiuzulu   Spika wa bunge la serikali ya Gabon Guy Nzouba Ndama ametangaza kuwasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia uchaguzi wa rais unaokaribia kufanyika nchini humo. Ndama aliarifu kuchukuwa uamuzi huo kutokana na mizozo ya … Read More
  • CUF waichana China kuhusu uchaguzi wa Zanzibar   CHAMA cha Wananchi (CUF) kimempuuza Dk. Lu Youqing, Balozi wa China nchini Tanzania, aliyesifia uchaguzi wa marudio Zanzibar uliofanyika tarehe 20 Machi mwaka, anaandika Regina Mkonde. Dk. Youqingal… Read More
  • Odinga amtembelea Magufuli Chato Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoan… Read More
  • TTCL Waiomba Serikali Kumilikishwa Mkongo Wa Mawasiliano Wa Taifa KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu Tanzania TTCL imeiomba serikali kuwamilikisha mkongo wa mawasiliano wa Taifa ilikampuni hiyo waweze kuuendesha wao kutokana na uwezo walionao na mafundi na wataalamu wa kutosha. … Read More
  • BUNGE kuanzisha kituo chake cha TV Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema uamuzi wa serikali kuzuia matangazo TBC kutokurusha moja kwa moja(live) matangazo ya Bunge ilikuwa na lengo la kulinusuru shirika hilo lisife kwan… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE