Abuja, Nigeria
Baada ya kukaa takribani miezi mitatu akipatiwa matibabu nchini
Uingereza hatimaye Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amewasili
katika mji mkuu wa Abuja na kupokelewa na viongozi wa ngazi za juu wa
taifa hilo wakiongozwa na Makamu wa Rais wa nchi hiyo.
Rais Buhari alikuwa katika matibabu kwenye moja ya hospitali nchini
humo ambapo alilazwa kwa takriban miezi mitatu. Hata hivyo haijafahamika Rais huyo alikuwa akiugua ugonjwa gani.
Hii ni mara ya tatu kwa kiongozi huyo kwenda Uingereza kwa ajili ya
kupatiwa matibabu. Jumatatu ijayo kiongozi huyo anatarajiwa kuhutubia
taifa hilo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment