Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
CHADEMA Mkoani Rukwa kimeshindwa kufanya ibada ya maombi kwa ajili ya
Mwanasheria Mkuu wa Chama chao, Mh. Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi
hivi karibuni baada ya polisi mkoani humo kuzuia ibada hiyo kwa kudai
ni mkusanyiko usio halali.
Mwenyekiti
wa CHADEMA mkoa huo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kanda, Sadrick
Malila amesema wamesikitishwa sana na hatua ya jeshi hilo kwani suala la
kumuombea mbunge huyo kamwe lisingeweza kusababisha uvunjifu wa amani
ndiyo maana alichukua hatua za kuomba kibali kwa Kamanda wa polisi mkoa
huo siku moja kabla.
Amesema kuwa CHADEMA mkoa ilikuwa
imewaalika viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali na wachungaji
walikuwa tayari wamejiandaa kwaajili ya maombi hayo, lakini wamelazimika
kusitisha baada ya Kamanda wa Polisi, George Kyando kuwaeleza kwamba
wasitishe.
"Jana nilimpigia simu
Kamanda wa Polisi na kumpa taarifa kwamba leo hapa ofisini tungekuwa na
ibada fupi ya kumuombea kiongozi wetu aweze kupata nafuu haraka ili
aweze kurejea kwenye majukumu yake na akawa ametukubalia, lakini cha
kusikitisha zaidi leo tukiwa tunajiandaa na na ibada hiyo na viongozi
wakiwa wameshawasili RPC akanipigia na kunijulisha tusitishe zoezi
hilo. Inaumiza sana kwani zoezi halikuwa la kisiasa" amesema
Aidha baada ya zuio hilo Mwenyekiti huyo
amelaani shambulio la Mwanasheria wao na kulitaka jeshi la polisi
limalize haraka uchunguzi na kuwatia mbaroni walioshughulika na tukio
hilo pamoja na wale waliomjeruhi ofisa wa jeshi kwa kumpiga risasi juzi
jijini Dar es Salaam ili kukomesha vitendo hivyo.
Malila pia aliwatangazia wanachama wa
CHADEMA na wananchi wengine waliokuwa na nia ya kumuombea Lissu kuwa
kila mtu afanye maombi binafsi kwani anaamini Mungu ni mwema na atajibu
maombi yao.
"Naliomba sana jeshi la
polisi kama wameshindwa kulinda raia na mali zao, basi waache kulinda
mali watalinda wananchi wenyewe wao wawalinde raia tu kwa kuwa
inawezekana majukumu yamewazidia wabaki na kitu kimoja na wanachi
wawasaidie kitu kingine. Jana wamezuia vjana wetu Dodoma wasichangie
damu wakati hospitali haina damu na hatujui wana maanisha nini." ameongeza.
Naye Katibu wa Baraza la Vijana CHADEMA, Julius Mwita amethibitisha kutokea kwa zuio hilo ambapo amesema kuwa " Hawakuwa
wanafanya mkutano wa siasa bali ni ibada maalumu ndiyo maana hata
viongozi wa dini wakaalikwa. Tunasikitika wameshindwa kufanikisha
kutimiza ibada hiyo kutokana na zuio la polisi".
0 MAONI YAKO:
Post a Comment