Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia kesi ya madai mzazi
mwenzie, Msanii Naseeb Abdul @diamondplatnumzkwa madai ya kushindwa
kumuomba radhi pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao, Abdul
Naseeb Juma.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa
@hamisamobetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya
Uwakili ya Century Attorneys.
Katika wito huo Diamond anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi, amesema mteja wao
Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka
apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
Shauri hilo linatarajiwa kutajwa ifikapo Oktoba 30, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

0 MAONI YAKO:
Post a Comment