October 08, 2017

Image may contain: 2 people, text 
Mkuu wa Wilaya Mh:Happyness Seneda akizungumza jambo
  
Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, imezindua Opereshini maalum ya kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa ki elimu.

Operesheni ondoa zero Kisarawe imezinduliwa rasmi jan tarehe 07/10/2017 na mhe. Suleiman Jafo mbunge wa Kisarawe na waziri mteule wa OR-TAMISEMI.

Akielezea kwenye uzinduzi huo, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happyness Seneda imegawanyika katika hatua mbili:  
 Image may contain: 3 people, people smiling, people standing and wedding 
Waziri mteule wa TAMISEMI Suleiman Jafu kulia ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo
 
1) Kuwaweka kambi wanafunzi wote Wa kidato cha nne kuanzia tarehe 1/10/2017 mpaka hapo watakapo maliza mitihani yao mwezi November. Hivyo fedha inahitajika kwa ajili ya malazi na chakula. Lakini pia tunapokea michango ya chakula moja kwa moja kama vile mchele, unga, mahindi, mafuta pamoja magodolo
2) Kukusanya michango kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya shule zetu za secondary kwa kujenga mabweni, vyoo, maktaba, madarasa , upatikanaji wa vitabu na ujenzi wa nyumba za walimu. Katika eneo hili, tunapokea fedha lakini pia materials mbalimbali kama vile bati, cement, nondo, tofali n.k
Jumla ya tsh. 65m zimekusanywa leo, na amesema kuwa Operesheni hii ni endelevu. 
Image may contain: 5 people, people smiling, people standing
Hivyo ameomba wadau mbalimbali waendelee kuunga mkono operesheni hii.
" tunamshukuru wadau wote waliojitokeza na kuchangia siku ya leo ya uzinduzi na hatimaye tumefanikisha kupata tsh 65m. 


              Image may contain: 5 people, people smiling, people standing 


Image may contain: 16 people, people smiling, people standing 



0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE