Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Edward Lowassa amemtembelea kumjulia hali mbungeSingida, Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibuNairobinchiniKenya.
Lowassa ameongozana mke wake Mama Regina Lowassa ambapo leo hii walifika hospitalini hapo kumjulia hali Mhe. Lissu.
Tangu picha za Lissu kuanza kuonakana pindi watu wanapoenda kumjulia hali, viongozi wa juu na wabunge wamekuwa wakifanya hivyo.
Miongoni mwao ni mbunge
wa jimbo la Tarime vijijini, Mhe. John Heche na mbuge wa Mbeya Mjini
Mhe. Joseph Mbilinyi ambao hivi karibuni wameonekana wakiwa katika picha
ya pamoja.
Tundu Lissu alipigwa
risasi akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma na watu wasiujulikana na sasa
anaendelea vizuri katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment