Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika mji mkuu wa India, New Delhi,
kabla ya kuanza safari ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
katika nchi hiyo.
Waandamanaji hao waliokuwa na ghadhabu wamekosoa vikali hatua ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani, ya kuitambua Quds Tukufu kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.
Baadhi ya vijana hao aidha wamechoma moto mabango yaliyokuwa na picha za Trump na Netanyahu.
Netanyahu anatazamiwa kuanza safari ya kikazi ya siku sita nchini India, licha ya New Delhi kupiga kura ya kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa la kupinga uamuzi wa Marekani wa kuitambu Quds kuwa mji mkuu wa Israel.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment