Mabalozi wa nchi 54 za Kiafrika katika Umoja wa Mataifa wamelaani
matamshi ya kudhalilisha yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani
kuhusu Waafrika
Mabalozi wa nchi 54 za Kiafrika wametoa
taarifa wakilaani matamshi ya kibaguzi na ya kudhalilisha yaliyotolewa
na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi za Kiafrika na Wamarekani
wenye asili ya Afrika na kumtaka aombe radhi na afute matamshi yake
hayo yenye kudhalilisha.
Trump Alhamisi iliyopita alizitukana
Haiti, El Salvador na baadhi ya nchi za Kiafrika kuwa ni "shimo la
kinyesi" na kutaka kusitishwa kuwapokea wahajiri kutoka nchi hizo.
Matamshi hayo ya Trump yamekabiliwa na jibu kali kutoka nchi mbalimbali
na jamii ya kimataifa ikiwemo Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa
Mataifa.
Hii si mara ya kwanza kuona matamshi ya
kigabuzi yanayotolewa na rais wa sasa Marekani dhidi ya wahajiri
yanazusha mjadala na kupingwa vikali. Tangu Donald Trump ashike hatamu
za uongozi, amekuwa akichukua hatua na misimamo ya kibaguzi dhidi ya
wahajiri, raia wenye asili ya Afrika na Waislamu, jambo lililosababisha
mivutano mikubwa ndani ya jamii ya Marekani na nje ya nchi hiyo. Patrick
Gathara mchambuzi mtajika wa masuala ya kisiasa wa Kenya amesema
kuhusiana na suala hilo kuwa: Matamshi hayo ya kibaguzi na kijahili ya serikali ya Marekani si jambo jipya.
Huko
nyumba pia Rais Trump alichukua uamuzi uliozusha mjadala mkubwa na
kupingwa sana pale alipowapiga marufuku kuingia Marekani raia wa nchi
saba za Kiislamu zikiwemo nchi tatu za Kiafrika. Trump anachukua hatua
hizo huku viongozi wa Washington wakitoa nara katika nyuga za kimataifa
kuwa wanaunga mkono haki za binadamu, kaumu na dini mbalimbali.
Trump
amechukua hatua kama hii dhidi ya nchi za Kiafrika na kujisahaulisha
kwamba hali ya aghalabu ya nchi hizo ikiwa pamoja na umaskini, machafuko
ya kisiasa na matatizo ya kiuchumi katika nchi hizo, ni matokeo ya
uingiliaji kati wa Washington barani humo kwa miaka kadhaa sasa.
Vilevile Trump mbaguzi anasahau au anajisahaulisha kuwa, raia wengi wa
nchi za Afrika wanaoishi Marekani kama wahajiri wametoa mchango mkubwa
katika maendeleo ya nchi hiyo. Wahajiri wengi na wale wanaotafuta
hifadhi wamelazimika kuhamia Marekani kutokana na siasa za nyuma ya
pazia za serikali ya Washington barani Afrika ukiwemo uungaji mkono wake
kwa makundi yenye misimamo mikali na ya kigaidi, lengo likiwa ni
kuvuruga amani na usalama na kupora maliasili na utajiri wa nchi hizo,
suala ambalo hatimaye huzisababishia nchi za bara hilo umaskini na hali
isiyoridhisha ya kimaisha.
Ukweli ni kwamba matamshi ya sasa ya
Trump yameibua wasiwasi miongoni mwa viongozi wa nchi za Kiafrika.
Matamshi hayo ya kichochezi na kibaguzi yanaweza kusababisha hatari
kubwa kwa raia wengi wa nchi za Kiafrika wanaoishi Marekani. Kwa msingi
huo matamshi haya ya sasa yameibua wimbi la hasira za viongozi wa
Kiafrika kadiri kwamba kitendo cha mabalozi wa nchi 54 za Kiafrika
katika Umoja wa Mataifa cha kuonyesha msimamo wazi wa pamoja na kupinga
matamshi ya kejeli na kudhalilisha ya Rais wa Marekani kinatajwa kuwa ni
cha aina yake.
Katika uwanja huo, Ras Mubarak mbunge wa Ghana anazungumzia suala hilo kwa kusema:
Nchi mbalimbali zinapasa kumtumia Trump ujumbe mkali kwamba walimwengu
kwa pamoja wanapinga na kupiga vita siasa hizo za chuki, za kuzusha
mifarakano na zisizo sahihi. Ingawa majibu makali yaliyotolewa
kikanda na kimataifa yamemfanya Trump akane kutumia na lugha hiyo chafu,
lakini viongozi wa Kiafrika wakiwa ni wawakilishi wa wananchi wa bara
hilo bado wanamtaka Trump awaombe radhi rasmi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment