Shehe akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu.
Hii ni laana! ndivyo unavoweza kusema baada ya kijana
mmoja aliyetajwa kwa jina la Dullah mkazi wa Chamwino, kibao cha shule Mkoani
hapa anadaiwa kufumaniwa akijaribu kumlawiti baba yake mzazi.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatatu iliyopita
Usiku nyumbani kwa mzee mmoja maarufu (jina linahifadhiwa kwa sababu za
kimaadili), anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 70.
Habari zinasema kijana huyo anadaiwa kumfanyia unyama
huo, baba yake ambaye alipiga yowe kuomba msaada
Akizungumza na mtandao huu, mzee huyo alisema kijana
aliyetaka kumfanyia unyama huo ni mtoto wake wa kumzaa lakini hivi sasa
ameathirika kwa ulevi, hivyo kama asingepiga yowe kuomba msaada angeweza
kutimiza haja yake ya kumlawiti.
"Huyu mwanangu alipofika hapa nyumbani alianza
kunipiga akidai kwanini napika chakula kidogo, ndipo alipojaribu kunivua suruali,
nilifanikiwa kumdhibiti asinilawiti" alidai mzee huyo
Andrew John ni mmoja shuhuda wa tukio hilo aliuambia Mtandao
huu.
"Huyu mzee ... anaishi chumba kimoja
na kulala kitanda kimoja na mwanaye huyo ambaye ni mlevi wa kutupwa
"Leo saa 2
usiku tulisikia mzee akipiga
kelele ndani kuomba msaada, tulidhani wamevamiwa na majambazi, tukakimbia na
kukuta mlango umefungwa, tulivunja mlango tulipoingia ndani tukamkuta kijana
wake amemkumbatia.
"Mzee huyo alidai kijana wake huyo alitaka
kumlawiti nasi tuliposikia hivyo tukamshushia kichapo Dullah, baadae
tukamwita kaka yake naye kwa hasira alitaka kumkata panga,
akatuponyoka na kutimkia kusiko julikana
Akizungumzia tukio hilo, shehe anayeishi mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Kudo Said
alisema siku hiyo, alikuwa kwa rafiki yake mmoja ambaye anafanya biashara ya
kuuza mabegi ndipo Dullah alipofika
akikimbizwa na watu wachache wakiwa wameshika mawe mkononi.
Alisema, aliwazuia wale watu wasimpige ndipo wakaanza
kumueleza kilichotokea kabla ya kumuomba amuombee dua
"Aliniambia yeye anakimbizwa na watu kwa sababu
anampenda baba yake.
Nikamuuliza
kivipi, au ni kweli alikuwa anataka kumlawiti baba yake kama wale waliokuwa
wana kukimbiza walivyosema, akasema hajamlawiti lakii nimuombee ili asirudie
tena basi mimi nikamuombea na baadae
akaondoka zake., alisema shehe huyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Tupendane Kata ya Chamwino,
Francis Sentimali siku ya tukio alikuwa mbali na eneo hilo,
lakini alipigiwa simu na kuelezwa kuwa
kumetokea tukio hilo na kwa kuwa alikuwa mbali, alishindwa kupata uhakika wa moja
kwa moja.
“Niliporudi nilifika na kuchunguza lakini sikupata jibu la moja kwa moja maana
pia hakuna aliyekuja kulalamika rasmi kwangu alisema mwenyekiti huyo, Alipoelezwa kwamba anachukua hatua gani kwa
matukio kama hayo kutokea katika mtaa wake na kwamba Mwandishi wa habari hizi
alishuhudia mlango wa mzee huyu ukivunjwa na watu waliofika kumpiga kijana
aliyetaka kumlawiti baba yake huyo Mwenyekiti alifunguka.
Kwanza niwatake watu wasichukue sheria mkononi, jamii
yetu pia ibadilike kwa kuacha kufanya matukio mabaya katika jamii yetu. Wazazi
tuwalee vizuri watoto wetu.
Na Dunstan Shekidele
0 MAONI YAKO:
Post a Comment