Producer mkongwe Bongo, P Funk Majani amefunguka kuhusu kuwepo kwa beef miongoni mwa ma-producer wapya wa sasa.P Funk ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wao kama ma-producer
wanaheshimiana na suala la malumbano mara nyingi ni kwa wasanii na si
kwao kwani kwa upande wa production wapo wachache.
“Labda hao wadogo ambao juzi kati nimeona wanalumbana, sijui S2kizzy,
T Touch na Luffa, sijui wanasema muziki wa T Touch wa kizamani, hitu
kama hivyo tunacheza taarab sasa,” amesema.
“Kwa sababu kinachoonekana ni kazi, kama muziki umekubali basi ni mzuri uwe wa kizamani au wa kisasa,” amesisitiza.
Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa ni ma-producer ambao kwa sasa kila
mmoja anafanya vizuri hapa Bongo, wote kwa sasa ngoma walizofanya
vinafanya vizuri katika radio station mbali mbali.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment