Baada ya wekundu wa msimbazi Simba kutolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na timu ya Al Masry huku wakitoka sare ya 0 – 0 nchini Misri, afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa timu yake imefanya kila kitu lakini mwisho wa siku mpangaji ni Mungu hata hivyo wanarejea nyumbani wakiwa wameacha heshima kubwa.
Tumefanya tuliyojaaliwa lakini mpangaji wa kila kitu ni Manani…jitihada hazishindi kudra..tunarudi nyumbani tukiacha heshma kubwa ya klabu na nchi kwa ujumla Misri…sasa nguvu yetu ipo ktk VPL…..Asante kwa dua na Sala zenu..Bravo SSC
Picha za matukio ya uwanjani nchini Misri
0 MAONI YAKO:
Post a Comment