Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amepingana na maamuzi ya
serikali ya kukataa kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa kudai kuwa
kuongeza mshahara kila mwaka kwa wafanyakazi ni suala la kisheria na ni
la lazima.
“Kupandisha mishahara ya Wafanyakazi ni suala la kisheria. Kiutaratibu Serikali inapaswa kupandisha mishahara kila mwaka kulingana na mfumuko ya Bei ili kulinda nguvu ya manunuzi ya Mfanyakazi. Vyama vya Wafanyakazi HAVIPASWI kukubali maelezo ya kisiasa.“ameandika Zitto.
Hata hivyo, Zitto amevishauri vyama vya Wafanyakazi nchini kupingana na maamuzi hayo ya serikali “Vyama vya Wafanyakazi havipaswi kukubali maelezo ya kisiasa”.
Kauli ya Mhe. Zitto Kabwe imekuja yakiwa ni masaa machache yamepita baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza kuwa serikali haitaongeza mishahara ya wafanyakazi kwa mwaka huu.Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 01, 2018 katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Iringa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment