Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Benki ya KCB wamesaini
mkataba wa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2018/19 wenye
thamani ya shilingi Milioni 420.
Udhamini
huo unakuja siku chache baada ya wadau wa soka kuhoji juu ya udhami wa
ligi hiyo baada ya wadhamini wa kuu kampuni ya simu ya Vodacom kumaliza
mkataba wao.
Hata hivyo Shirikisho la soka nchini halijaeleza
hatua iliyofikia mpaka sasa na mdhamini mkuu Vodacom baada ya kuelezwa
kuwa ipo katika mazungumzo na kampuni hiyo juu ya kuongeza mkataba.
Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 inatarajia kuanza Agosti 22 ambapo tayari ratiba ya msimu mzima imeshatoka.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment