MwanaMmuzki kutoka mkoani Morogoro na kada wa Chama cha Mapenduzi, Selemani Abdallah Mutabazi Msindi Afande Sele kupitia ukurasa wake wa Facebook leo hii, amemtambulisha mtoto wake wa Kiume wa pakee anayeishi Jijini Mwanza Tanzania. Afande Sele amepa jina la Majiani mtoto huyo akitoa heshima kwa Producer P.Funk kwa mchango mkubwa katika mziki wake.
Majani Selemani Msindi
"Ktk maisha yangu ya muziki niliweza kufika Mwanza mara nyingi zaid
kuliko mkoa wowote ndani ya nchi yetu...lkn ukiniuliza ni kitu gani
ninachojivunia kutoka Mz nje ya kufanya show za mziki na kukubalika
kupita kiasi?....Jibu langu ni rahisi tu kwamba nilibahatika kumpata
huyu mvulana mdogo mwenye miaka kumi sasa hivi ambae tangu akiwa tumboni
mwa mama yake nilimpa jina la Majani kama heshima kwa producer wangu wa
kihistoria aliyechangia kiasi kikubwa kufanya mimi niwe
mwanamuziki...Huyu ndio kaka pekee wa kina Tundajema na
Ahsantesanaa....yeye ndio mrithi wangu wa baadae....Majani Selemani
Msindi...."
Mtoto huyo wa kiume ndiye anakuwa kaka pekee wa watoto Tundajema Selemani na Asantesanaa Selemani Msindi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment