
Wakati huo huo kanali ya televisheni ya wapiganaji wa Kihouthi imetangaza kuwa vikosi vya jeshi la Yemen vilifyatua risasi wakati vikipiga doria katika ikulu ya rais, hatua iliyosababisha ghasia. Mivutano imekuwa ikishadidi huko Yemen kati ya wapiganaji wa Ansarullah wanaojulikana pia kwa jina la Mahouthi na vikosi vya serikali, baada ya wapiganaji hao wa Kishia kumtia mbaroni Ahmed Awad bin Mubarak, mkurugenzi wa ofisi ya Rais Abdrabuh Mansour Hadi wa Yemen. Mubarak alitiwa nguvuni katika kituo kimoja cha upekuzi katika mkoa wa Hada kusini mwa Yemen.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment