April 06, 2015

Mwanamke mmoja, Kudra Janja  mkazi wa  Kijiji cha Bwai, wilayani Butiama mkoani Mara amelipuliwa kwa petroli na mumewe, Simon Otieno  kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.Katika tukio hilo pia mtoto aliyejulikana kwa jina la Tatu Simon (1) alifariki dunia muda mfupi baada ya kuungua kwa moto katika unyama huo uliofanywa na baba yake mzazi.

Habari kutoka katika kijiji hicho zinasema kwamba mume wa mama huyo, Simon aliamua kuwamiminia petroli mke na mtoto wake kupitia dirishani kisha kulipua kwa moto chumba ambacho wawili hao 

 
walikuwa wamelala Machi 31, mwaka huu.

Kudra ameungua vibaya mwili mzima na alilazwa katika Hospitali  ya Mara na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza wakati mtoto wake alikutwa ndani ya nyumba hiyo akiwa ameungua vibaya na baadaye kufariki dunia.

Mama mdogo wa Kudra  aliyejitambulisha kwa jina la Bahati Magesa aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mjomba wao saa 10 usiku.“Kisa cha tukio hili ni ugomvi wa siku nyingi unaotokana na wivu wa mapenzi kwa watu hawa ambao wameishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja tu,” alisema Bahati.

“Otieno alikuwa akimtuhumu mke wake kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wengine lakini baadaye ugomvi huo uliisha na wakawa wanaendelea na maisha yao vizuri.“Baada ya tukio hili Kudra ambaye ni mtoto wa dada yangu aliniambia kuwa mumewe aliingia ndani akiwa na dumu la petroli na alipomuuliza la nini alimuambia alale, halimhusu.

“Baadaye alimwaga mafuta dirishani akachukua kibiriti na kutoka nje akawasha na kuacha mlipuko mkubwa na yeye kutokomea kusikojulikana.“Baada ya moto kulipuka, Kudra alipiga yowe ndipo mjomba wake, Obadia Janja alikimbilia na kwenda kumuokoa na akamtoa nje na mtoto wake wakati moto unawaka kwa kasi.

“Mama alikuwa ameungua mwili mzima na mtoto aliungua vibaya sana na baada ya muda mfupi aliaga dunia,” alisema Bahati.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 “Tumeanza kumtafuta Simon Otieno ambaye amefanya tukio la kinyama na linapaswa kulaaniwa na kila mmoja. Ninaiomba jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi,” alisema Kamanda Kalangi

Related Posts:

  • Kuhusu hirizi ya Chege na kumshambulia ,Maumartha naye ajibuBaada ya Chege kumbwatukia Maimartha aliposema amevaa hirizi kule dodoma kwenye shoo maimartha aamua kumtolea uvivu vhege na kufunguka instagram kama ifuatavyo @chegechigunda this is too much embu koma kunitukana mpuuzi ni we… Read More
  • Msiba:Kapten John Komba amefariki dunia    Mbunge wa Mbinga  Mh: john Komba, amefariki Dunia jioni hii. Taarifa za kifo cheke zimetolewa katika A/C ya Twitter ya CCM na kusambaa katika vyombo mbalimbali .    Kepteni Komba enzi za uha… Read More
  • Chenge, Ngeleja, Tibaijuka OutKamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi kimewasimamisha ujumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho NEC wanachama wake watatu ambao ni wajumbe wa NEC kufuatia na kuhusika kwao katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow. Wajumbe hao ni m… Read More
  • Diamond atajwa kuwania tuzo nyinge kubwa Africa Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo za 16 za Vodafone Ghana Music (Awards), VGMA 2015. Majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo yametajwa kwenye hoteli ya La Palm Royal Beach Hotel jijini Accra, jana Ijumaa, Februar… Read More
  • Nisha afunguka uhusiano wake na Nay ndani ya Papaso    Msanii wa Filamu nchini, Salma Jabu maarufu Nisha, ameongea mambo mengi kuhusiana na sanaa yake, wasanii  na mahusinao yake ya kimapenzi na msanii Nay wa Mitego. Akizungumza na D'Jaro Alungu ndani ya Pap… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE