March 19, 2016

                                         
                                   Rais wa club za waandishi wa habari tanzania(utpc)

Mwandishi wa habari Bi. Salma Said,anaedaiwa kutekwa na watu siojulikana kwenye uwanja wa Mwalimu Julias Nyerere

Salma Said mwandishi wa DW Zanzibar ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es salaam, hali ambayo imeleta fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia yake  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marejeo Zanzibar.
Ifahamike kuwa Kazi  ya mwandishi wa habari ni kutoa habari juu ya kila kinachoendelea katika jamii , hivyo kama kuna dosari , dosari hiyo ni ya jamii na sio ya anayeieleza dosari .
UTPC inalaani na kupinga utekaji uliofanywa ambao sababu zake bado hazijulikani, hivyo tunaitaka serikali kuhakikisha Salma Said anatafutwa, kupatikana  na anaachiwa huru mara moja kwa kuwa Serikali ndio yenye jukumu la kulinda raia wake.
Kama utekwaji wa Salma umefanywa kutokana na kazi yake ya uandishi habari tunalaani vikali hatua hiyo, vitendo hivi havipaswi kuendelea katika  nchi inayoheshimu misingi haki na Demokrasia, Vitendo vya namna hii vinadumaza na kufifisha  uhuru wa habari .
Tunapinga kwa nguvu zetu zote  waandishi wa habari kukamatwa na vyombo vya dola au makundi ya kihalifu kwa visingizio ama vya uchochezi au maslahi ya taifa.
Waandishi tutaendelea kufanya kazi zetu bila kujali vitisho vya aina yoyote ile kutoka kwa mtu yoyote au Serikali.
Imetolewa na
DEOGRATIUS NSOKOLO
RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC.
March 19, 2016

Related Posts:

  • Gari la kikosi cha Zimamoto limevunjwa vioo   Picha hii siyo halisi ya tukio   Jeshi la Polisi mjini Tunduma mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliofunga barabara. Akiongea na East Africa Radio kwa njia ya simu Kaman… Read More
  • Umeipata hii ya majaji 3 kufutwa kazi kwa kutazama video za ngonoMajaji watatu wamefutwMajaji watatu wamefutwa kazi kwa kutumia muda wao afisini kutizama filamu za ngono. Jaji Timothy Bowles anayesikiza kesi za wilaya , jaji wa maswala ya uhamiaji Warren Grant na jaji Peter Bullock wamefut… Read More
  • Makinda: Zitto Kabwe ni mbunge halali   Spika wa Bunge Mh Anne Makinda amesema kuwa kwa niaba ya Bunge bado anamtambua mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuwa ni mbunge halali wa bunge hilo. Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya kikao… Read More
  • Makamu wa rais wa afutwa kazi    Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo.Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kump… Read More
  • Waumini 10 wa dini ya kikristu wazikwa    Wakristu wazika wapendwa wao waliouawa katika milipuko makanisani Waumini wa dini ya kikristu nchini Pakistan wamekusanyika kwa maziko ya waathiriwa wa mauaji ya siku ya jumapili yanayoaminiwa kufanywa na … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE