July 17, 2016

2
Baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa kuwa halikuzuia mikutano ya ndani ya vyama na kuwa kilichozuiliwa ni mikutano ya hadhara namaandamano, Baraza la Vijana CHADEMA wamekuja na mbinu nyingine ya kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa CCM Julai 23 hautafanyika.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe aliwataka BAVICHA kutokwenda Dodoma kwa madai kuwa wamejionea kuwa Jeshi hilo linaupendeo na kuwa limeegemea upande mmoja.
BAVICHA wameeleza kuwa wanatarajia kufanya mkutano Julai 20 mkoani Dodoma ambapo watapanga nini cha kufanya ili mkutano huo usifanikiwe kwani wameona Polisi hawana dalili za kuuzuia mkutano huo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa BAVICHA alisema kuwa, wakati mwingine mkubwa wako akisema kitu hata kama hukifurahii inabidi tu ufanye. Aliyasema hayo akinukuu kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA aliyewataka kutupilia mbali mpango wa kwenda Dodoma.
Inaelezwa kuwa BAVICHA walikuwa wamewaandaa vijana zaidi ya 4,000 ambao wangekwenda kulisaidia Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa CCM haufanyiki.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE