
Hatimaye klabu ya Yanga imefanikiwa kumsajili rasmi kiungo mkabaji kutoka Zambia, Justine Zulu kwa mkataba wa miaka miwili.Kiungo huyo anaungana na kocha wake wa zamani aliyekuwa anamfundisha kwenye timu ya Zesco United ya Zambia, George Lwandamina aliyesajiliwa kuifundisha Yanga siku chache zilizopita.
Zulu mwenye miaka 27 amewahi kuchezea timu kadhaa ikiwemo National Assembly, Hapoel Be’er Sheva, Hapoel Bnei Lod, Hapoel Rishon LeZion, Enosis Neon Paralimni, Lamontville Golden Arrows, Kabwe Warriors na ZESCO United.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment