July 13, 2017

 
Mwanamuziki wa R and B Tanznaia  Rama Dee, amewaomba Radhi mashabiki wa Clouds Fm na Clouds Media kwa pamoja kwa yale yaliyotokea kipindi cha nyuma. Kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm akiitambulisha wibo wake mpya Rama dee ameomba msamaha na kukili kwamba yalioyopita yamepita

 “Mimi nasema kwa mashabiki wangu wote wa Clouds Fm na kote wanakonisikiliza, sasa hivi ni muda wa sisi kukaa sehemu moja. Kwa hiyo, kwa chochote ambacho kimetokea kwa Rama Dee ambacho kilionekana si sahihi, naweza kusema I m sorry” amesema Rama Dee na kuongeza.
“Na kwa Clouds Fm kwa wao wenyewe wanaona kwamba kuna sehemu walinikosea, tayari tumeshazungumza na tumeshamaliza kwa hiyo tupo sehemu nzuri na bila shaka upendo uendelee,” alimaliza kwa kusema.

 Ikumbukwe kuwa Rama Dee ndiye aliyekuwa akifanya chorus katika ngoma za ‘kundi’ la Anti-Virus ambalo lilitoa albamu za kukishambulia kwa maneno kituo hicho cha radio, hata hivyo Rama Dee amesema katika albamu zilizotoka hakuna sehemu aliyotukana.

Bofya Video kutazama Interview hiyo
                 

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE