November 16, 2017

Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera ameibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika jumapili. Bi Bujinginya, mama wa watoto wawili ambaye anaungana na washindi milioni 130 wa TatuMzuka amesafirishwa kwa ndege kutoka Ngara kuja Dar es Salaam ili kuchukua pesa yake ya ushindi katika mkutano na waandishi wa habari.
Akizungumzia ushindi huo, Bujinginya alisema,“Baada ya kuishi kwa kutafuta pesa ya mlo kila mwezi na miezi mingine bila pesa, Kiukweli sikujua itakavyokuwa ikifika Januari. Nimefurahi sana kwamba sasa naweza kutembea kwa kujiamini tena baada ya ushindi huu.”
Pia katika tukio la kukabidhi zawadi kwa mshindi alikuwepo Bwana Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.Dhamira ya Tatu Mzuka ya kubadilisha maisha ya watu haijabadilika ambapo zimebaki siku chache ili ichezeshwe droo kubwa ya Supa Mzuka jackpot ya milioni 150 jumapili ijayo. Tarehe 19 Novemba saa 3:30 usiku Mtanzania mmoja ataondoka na kitita cha milioni 150.
“Kila mtu ambaye umecheza tangu Tatumzuka izinduliwe na kutumia kuanzia shilingi 500 tu kupitia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, umeingia katika droo hii ambapo unaweza kujishindia milioni 150,” alielezea mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba.
Bi Mutahaba aliwahimiza watanzania kuendelea kucheza, akisisitiza kwamba bado washiriki hawajachelewa kujiwekea nafasi ya ushindi huo wa kihistoria.
Pichani kulia ni Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera akizungumza jana jijini Dar mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyoibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki.Pichani kati ni mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akiwa pamoja na Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.
 
Pichani kati ni mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akiwatambulisha Washindi wa mchezo  huo, mbele ya Waandishi wa habari mapema jijini Dar.
 
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera alieibuka  mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka  ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 
 
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi, Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE