February 15, 2014

Mwimbaji nyota wa pop, Christina Maria Aguilera ataikumbuka vyema siku maalum ya wapendanao ya mwaka huu (February 14, Valentine’s day) kwa tukio kubwa lililompa furaha na kumpigisha hatua nzuri katika maisha yake ya mapenzi.
Mwimbaji huyo alichumbiwa na boyfriend wake, Matthew Ruther ambaye ni mtayarishaji wa filamu. Christina alishare picha inayoonesha pete aliyovishwa akiwa ameshikiliwa mkono na mchumba wake huyo na kuandika, “He asked and I said…”
Mwimbaji huyo mzaliwa wa New York, Marekani aliwahi kufunga ndoa na Jordan Bratman November 19, 2005 lakini ndoa hiyo haikudumu na walilazimika kuachana rasmi April, 2011 wakiwa tayari wana mtoto mmoja wa kiume, Max Bratman.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE