Miezi kadhaa iliyopita klabu ya Chelsea ilithibitisha rasmi kwamba haitomuongeza mkataba mpya mchezaji Ashley Cole ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2003 akitokea Arsenal. Baada ya taarifa hiyo timu nyingi zikaanza kuhusishwa na usajili wa mchezaji huyo.
Leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo amejiunga rasmi na AS Roma ya Italia.
Cole ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa £185,000 kwa wiki na Chelsea amekubali kukwata kiasi cha £160k kwa makubaliano ya kulipwa kiasi kisichozidi £35,000 kwa wiki na klabu hiyo ya Serie A.
Ashley Cole amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Rome
0 MAONI YAKO:
Post a Comment