August 15, 2014

 
Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Khamis Kagasheki akizungumza jambo na baadhi ya wasanii muda mfupi baada ya kukutana Josiah Girls High School iliyopo mjini hapo mapema leo.
 
Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Khamis Kagasheki akizungumza jambo na baadhi ya wasanii muda mfupi baada ya kukutana Josiah Girls High School iliyopo mjini hapo mapema leo.
 
Kagasheki akitoa wasaha mfupi kwa Wanafunzi hao muda mfupi kabla ya kufunga ziara hiyo fupi.
 
Mmoja wa wanafuzi wa shule hiyo akiwaonyesha wasanii baadhi ya kazi za masomo wanazofanya kila siku.
 
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (kulia), akiongozana na wasanii hao kuingia kwenye moja ya jengo la shule hiyo tayari kwa kujionea baadhi ya shughuli za masomo yao zinavyokwenda.
 
Wasanii hao wakiingia shuleni hapo muda mfupi baada ya kuwasili.
 
Recho akiimba moja ya kipande cha nyimbo yake ya Kizunguzungu mbele ya wanafunzi hao.
 
Baadhi ya madereva wa magari ya Serengeti Fiesta 2014 wakijadiliana jambo shuleni hapo.
 
Wanafunzi hao wakifuatilia baadhi ya maneno waliyokuwa wakipewa na wasanii hao.
 
Baadhi ya wasanii wakicheza muziki na wanafunzi hao.
 
Mwenyekiti wa kamati ya Serengeti Fiesta 2014 Sebastian Maganga akiongea jambo kwa niaba ya wasanii na viongozi wote walioambatana na msafara wa Fiesta Bukoba.
 
Nay wa Mitego akiimba moja ya wimbo wake mbele ya wanafunzi hao.
 
Baadhi ya wanafuzi hao wakionyesha uwezo wao katika kucheza muziki.
 
Linah akiongea jambo kwa wanafunzi hao.
 
Baadhi ya wanafunzi na viongozi wa shule hiyo wakiwa kwenye pozi la pamoja na timu ya Serengeti Fiesta 2014 iliyokuwa imewatembelea shuleni hapo.

MBUNGE wa Bukoba Mjini, Mhe. Khamis Kagasheki leo alipata fursa ya kukutana na Bbaadhi ya wasanii wa Bongo Fleva waliopo kwenye ziara ya Serengeti Fiesta 2014 Bukoba kwa kuwatembeza katika shule ya wasichana ya Josiah Girls High School ya mjini hapa, ambayo hivi karibuni ilifanya maajabu kufaulisha wanafunzi wengi mtihani wa kidato cha sita.
Akizungumza mbele ya wasanii na wanafunzi wa shule hiyo, Kagasheki alisema kuwa amefarijika sana kupata fursa ya kukutana na wasanii watakaofanya shoo usiku wa leo katika Uwanja wa Kaitaba, kwani ni jambo la kipekee kabisa kwa uamuzi wao wa kutembelea shule hiyo kabla hawaingia uwanjani kufanya makamuzi yao.
Wasanii waliofika shuleni hapo walipata fursa ya kuimba vipande vya nyimbo zao na kutembelea baadhi ya madarasa na mabweni ya shule hiyo na baadaye waliona vipaji vya wanafunzi hao katika kucheza na kuimba.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL, Bukoba)

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE